MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA LEVIS MLENGA (43) MKAZI WA LUFITA NCHINI MALAWI
ALIFARIKI DUNIA AKIWA AMEFUNGIWA KATIKA CHUMBA KIMOJA KATIKA OFISI YA
KATA BAADA YA KUPIGWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI WA NG’OMBE WAWILI MALI YA EMMANUEL KILEMBE,
MKAZI WA KIJIJI CHA ILONDO.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 06.09.2014 HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA
MALANGALI, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA
KUWA MAREHEMU ALIKAMATWA NA ASKARI POLISI WA NCHINI MALAWI NA
ALIPOJARIBU KUTOROKA NDIPO WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMKIMBIZA NA
WALIPOMKAMATA WALIANZA KUMSHAMBULIA NA KUMSABABISHIA MAJERAHA SEHEMU ZA
KICHWANI HALI ILIYOPELEKEA KUTOKWA DAMU PUANI NA MDOMONI.
AIDHA,
WATU WATATU WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. EMMANUEL
KILEMBE 2. ITISON NDIMBWA WOTE WAKAZI WA ILONDO NA 3. FURAHA KIBONA,
KAIMU MTENDAJI KATA YA MALANGALI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA – ITUMBA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
WATU WANNE
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MORTINA (30) 2. EDINA JASON (22). 3.
PAULO MWANYALILA, PADRI KANISA LA ROMANI CATHOLIC KYELA NA MWANAMKE
MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE MARA MOJA WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA MAGARI MAWILI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.241 BKZ AINA YA TOYOTA
COASTER IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE
KUGONGANA NA GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI IKIENDESHWA NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 08.09.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO MAENEO YA GARIJEMBE, KATA YA UTENGULE, TARAFA YA BONDE
LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
MBEYA/TUKUYU. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU WALIJERUHIWA AMBAO NI
1. SAMWEL ASANGA (34) 2. MAWAZO GASPER NA 3. MTOTO WA KIUME, UMRI KATI
YA MIAKA 02 – 03 AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE.
CHANZO
CHA AJALI HIYO BADO KINACHUNGUZWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO.
MADEREVA WA MAGARI YOTE MAWILI WALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI HIYO,
JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO WA MIAKA MIWILI (02) ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GROLIA LEVOKATUS MKAZI WA ITEWE AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 08.09.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO
ITEWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA
JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU NA
WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
IKIWA NI PAMOJA NA KUVUTA MAENEO YENYE VIVUKO. AIDHA ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA [MADEREVA] AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni