NA
SYLVESTER DAVID
MWANDAAJI
maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini,Emanuel Mkono‘Nah Reel’amekiri kuwa na
uwezo mkubwa katika uandaaji wa muziki kutokana na kazi alizozifanya na wasanii
mbalimbali wakubwa nchini.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima jana Jijini Dar es salaam kuhusu
mabadiliko ya muziki nchini,alisema mabadiliko ni makubwa sana na yuko katika
hatua za kuleta muziki mzuri katika soko la muziki nchini.
Nah
Reel ambaye ni mwandaaji aliyefanya kazi katika studio za Kama Kawa Record,Home
Town Record,Switch Record na sasa katika studio yake ijulikanayo kama ‘The
Industy’.
Aliwataja wasanii aliofanya nao kuwa ni wengi wakiwemo Kundi la Weusi,Vanessa Mdee, Diamond Platnum,Bonta,Kundi la Navy Kenzo,Izzo Busness,Kundi La Pah One,Mwana Fa,Roma,Kalla Jelemaya,Baba Levo,Rama D,Mapacha(Maujanja Suplayaz),Gosby,Quick Racka na Shilole.
Pia aliwataka mashabiki wa muziki wake nchini wategemee kazi nzuri na zenye ubora kutoka kwake na studio yake ya ‘The Industry’.
PICHA ZA BAADHI YA WASANII ALIOWAHI FANYA NAO KAZI
QUICK RACKA
DIAMOND
IZZO BIZNESS
SHILOLE
VANESSA MDEE
WEUSI
0 comments:
Chapisha Maoni