Text Widget

Recent Posts

Septemba 21, 2014

SHULE ZAFUNGWA DAR KUHOFIA WATOTO KUTEKWA

1Uvumi wa kuwapo kwa watu wanaoteka nyara watoto kwa kutumia magari aina ya Noah, umeleta mtafaruku katika shule saba za msingi Manispaa ya Temeke, na kusababisha wazazi kuvamia shule hizo na kufungwa kwa muda.
Hata hivyo, katika baadhi ya shule hizo kumeripotiwa kutokea vurugu kiasi cha jeshi la polisi kuingilia kati kutawanya watu waliotaka kuvunja mageti ya kuingilia kwenye shule hizo.
Taarifa za kuwapo kwa matukio ya watoto kutekwa na watu wasiojulikana zilianza kuenea wiki tatu zilizopita, ambapo shule zilizoathirika ni Chekeni Mwasonga, Mikwambe, Rangi Tatu, Mchikichini, Charambe, Kiburugwa, Jitihada na Mbagala Kuu.
Akizungumza na NIPASHE Jumamosi, Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba, alisema uvumi huo siyo wa kweli na hawafahamu nani anahusika kuusambaza na kwa madhumuni gani.
Alikiri kwamba kazi ya utoaji huduma katika baadhi ya shule umekuwa mgumu baada ya wanafunzi kutofika shuleni kufuatia  wazazi wao kuwazuia wakihofia usalama wa watoto wao.
MATUKIO YALIVYOJIRI
Mumba alisema taarifa ya kuwapo kwa watu wanaoteka nyara zilianzia katika Shule ya Msingi Mwasonga, ambapo ghafla zilisambaa kwa kasi kutoka shule moja hadi nyingine kiasi ambacho sasa inakuwa ngumu kudhibiti.
Imearifiwa katika matukio hayo kila shule kuna watoto kati ya wanne hadi sita walitekwa nyara katika mazingira ya kutatanisha na watu wasiojulikana ambao wanatumia magari ya Noah kwa ajili ya kutimiza vitendo hivyo.
“Hata mimi nashangaa uvumi huu unavyoenea kwa kasi na kusababisha kazi ya utoaji elimu kuwa ngumu, tunajitahidi sana kuwaelimisha wazazi lakini kila siku shule moja hadi nyingine inaathirika,” alisema.
Alisema Uongozi wa Manispaa ya Temeke kwa sasa unashirikiana na walimu na Jeshi la polisi, kuhakikisha wanajitahidi kutuliza taharuki katika shule hizo.
WALIMU WAKIRI HALI NI MBAYA
Wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili, baadhi ya walimu na viongozi wa serikali za mitaa, walisema hali imekuwa mbaya katika shule hizo baada ya wanafunzi kutohudhuria masomo kufuatia wazazi wao kuwazuia.
Mwenyekiti wa mtaa Rangitatu, Said Pazi, alisema toka siku ya Jumatatu ilipotokea tukio hilo, hali imekuwa ya wasiwasi kwa wanafunzi hao, ambapo baadhi yao wameshindwa kuhudhuria masomo kikamilifu.
Alisema siku ya tukio, kulikuwa na wakati mgumu baada ya wazazi waliokuwa na taharuki kuvamia shule hiyo na kutaka kuvunja geti kuu la kuingilia ndani, kushinikiza wapewe watoto wao baada ya kusikia kuna wanafunzi watatu wametekwa nyara.
“Nikiwa hapa ofisini wananchi walikuja na kuniambia kuna watoto wametekwa, lakini kila nikijaribu kuuliza mazingira ya tukio hilo, hakuna aliyeweza kueleza kwa usahihi, hata hivyo idadi ya watu ilipozidi kuongezeka na kuhatarisha amani ilibidi tuwaite polisi watusaidie,” alisema Pazi.
Kwa upande wa shule ya msingi, Jitihada ilibidi ichukuliwe hatua ya kufungwa shule kwa siku moja baada ya wazazi kuamua kuwachukua watoto wao kwa nguvu na wengine kukimbia ovyo baada ya kuenea taarifa ya kutekwa wanafunzi sita.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Odenary Mosha, alisema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 4.30 asubuhi, wakati wanafunzi wakiwa mapumziko.
Alisema walijaribu kuwatuliza wazazi hao, lakini ilishindikana baada ya kuanza kuvamia madarasa kwa nia ya kuwatafuta watoto wao.
Hata hivyo, Mosha alisema hakuna mwanafunzi aliyeripotiwa kupotea na hata mzazi aliyefika kusema mtoto hajarudi nyumbani kwao. Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kiburugwa, Mponda Shabani, alisema kwa ujumla wanafunzi wake wote 3,400 wapo salama na hakuna taarifa yoyote ya kupotea miongoni mwao.
Hata hivyo, Afisa Elimu mama Mumba, aliwashauri wazazi kuacha kusikiliza maneno ya mitaani na kueleza katika shule zote kunafanyika zoezi maalum la utoaji wa elimu wa kujitambua kwa wanafunzi.
DC: SINA TAARIFA

0 comments:

Chapisha Maoni