Muimbaji
wa Tip Top Connection, Madee hivi karibuni alijikuta katika wakati
mgumu baada ya kuwekwa ndani katika kituo cha polisi cha Kigamboni
kutokana na madai ya kuhusishwa na tukio la utekaji.
Kabla
ya kuongea na meneja wa kundi hilo, Babu Tale, mtangazaji wa Clouds FM,
Soudy Brown aliripoti kupitia ‘You Heard’ ya XXL kuwa Jumamosi
iliyopita Madee aliporwa simu yake na watu wawili usiku huko Kigamboni’
Babu Tale alisema: Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora,kwahiyo ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki halafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma. Pikipiki ilivyodondoka yule aliyekua nyuma kwenye pikipiki ambaye ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata aliyekuya anaendesha hiyo pikipiki.
“Wakamchukua
na kwenda nae maskani TipTop,” ameeleza Tale. Mama yake akaja akasema
‘msipeleke polisi mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu.
Madee kwa sababu alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake,
saa nne asubuhi yule mama akaja na polisi badala ya kuja na mwizi,
mwenzake akaja na polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu
pale Tiptop. Walimchukua huyo mhalifu kwenye Land Rover mpaka Polisi
Magomeni na kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa.”
“Alipigwa
akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka hospitali. Nikapigiwa simu na
Madee kwamba anatakiwa polisi akaripoti, kufika kituoni wakakuta ile
pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka hospitali akawaambia
‘huyu ni mwizi ameiba’ Ikabidi dogo aingizwe ndani jana akalala pale
olisi Magomeni.
“Asubuhi
yake Madee akaenda kituoni kama kufuata mhalifui wake na kutaka simu
yake aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe Kigamboni. Saa kumi
na mbili jioni ndio Kwebe ananitumia meseji anasema Madee analalamika
mbona humfatilii, nikauliza ‘kuna nini tena’ akasema wamemuingiza ndani.
Nikapiga simu polisi Kigamboni ndio wakaniambia kijana wako tulitaka
kumtoa lakini hatuwezi sababu amemteka mtu. Nikapiga simu kwenye vyanzo
vyangu vya msaada tukamtolea dhamana, ni hilo, yataisha kama
yalivyoanza’
Bongo5 leo imemtafuta Madee aliyesema yupo vizuri ila kwa sasa hawezi kuongelea kitu chochote kuhusu tukio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni