Text Widget

Recent Posts

Agosti 06, 2014

Wananchi wakili Mdahalo umetufunza




Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akizungumza kwenye mdahalo wa Katiba, uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi

  • Wakati waliohudhuria mdahalo huo Dar es Salaam walikuwa kila mara wanawakatisha watoa mada kwa makofi na vibwagizo vya “CCM, CCM, CCM” na “Babu, Babu, Babu”, katika mikoa mbalimbali watu walikusanyika katika maeneo mbalimbali ya vijiweni, baa, madukani kusikiliza huku wengine wakibeba redio na simu za mkononi
  •  

    Dar/ Mikoani. Mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa juzi na ITV umeelezwa kuwa uliotoa mafunzo makubwa kwa watu wengi katika maeneo mbalimbali nchini kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
    Wakati waliohudhuria mdahalo huo Dar es Salaam walikuwa kila mara wanawakatisha watoa mada kwa makofi na vibwagizo vya “CCM, CCM, CCM” na “Babu, Babu, Babu”, katika mikoa mbalimbali watu walikusanyika katika maeneo mbalimbali ya vijiweni, baa, madukani kusikiliza huku wengine wakibeba redio na simu za mkononi
    Mjini Dodoma, wananchi katika maeneo ya Mitaa ya Nyerere Square, Soko la Dk Rehema Nchimbi na viwanja vya Bunge, walishindwa kuvumilia na kujikuta wapiga kelele za juu katika mada iliyokuwa ikitolewa Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu umuhimu wa kupata Katiba Mpya.
    Moshi
    Makundi ya wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi wa kawaida walionekana wakifuatilia mdahalo huo uliomhusisha Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wengine.
    Wakati mjadala huo ulipoanza tu, watu mbalimbali walionekana kupigiana simu na wengine kutumiana meseji wakihimizana kuufuatilia.
    Mmoja wa waliofuatilia, Christopher Shayo ‘Kimeta’, alisema baada ya kumalizika kwa mdahalo huo ameweza kujua pumba ni zipi na mchele ni upi.
    “Sijui kama hawa viongozi wa CCM na wajumbe wao wa Bunge la Katiba waliuangalia, lakini kwa kweli wameumbuka mchana kweupe. Upotoshaji wao ulifikia tamati jana,” alisema Shayo.
    Mfanyabiashara, Festo Minja alisema ufafanuzi uliotolewa na wajumbe wa Tume unapaswa kuwa dira ya majadiliano kwa wajumbe wa Bunge la Katiba lililoanza jana bila maridhiano.
    Bukoba
    Mchuuzi, Derick Edmund anayeuza bidhaa karibu na Hospitali ya Mkoa wa Kagera alisema amefahamu mambo mengi baada ya kufuatilia mjadala huo.
    Alisema hoja zilizotolewa na Jaji Warioba kutetea Rasimu ya Katiba ndizo zilizomvutia zaidi na kusema kwa mvutano uliopo sasa itakuwa vigumu kupata Katiba Mpya hivi karibuni.

0 comments:

Chapisha Maoni