Text Widget

Recent Posts

Agosti 08, 2014

Mbunge Chiku Abwao ajibu mapigo



Chiku AbwaoMBUNGE wa Viti Maalum, Chiku Abwao (Chadema), amewashukia wanaomzushia kuwa amewasaliti wenzake wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), na kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea mjini hapa.
Habari za mbunge huyo, zilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari zikielezea kuwa ameonekana viwanja vya Bunge kwa malengo ya kuhudhuria vikao hivyo.
Kutokana na taarifa hizo, Abwao amekanusha vikali habari hizo na kusema, licha ya yeye kuwa masikini lakini hawezi kubabaishwa na viposho ambavyo serikali inawalipa wabunge wa bunge hilo kwa ajili ya kuwasaliti wananchi kwa kukanyaga na kudharau mawazo yao waliyoyatoa wakati wa ukusanyaji wa maoni juu ya katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, alisema yeye kama mwanasiasa mkongwe na mwenye uchungu wa kutetea watanzania, kamwe hawezi kuwasaliti wao na msimamo wa Ukawa.
Aidha, alisema anasikitishwa na serikali ya CCM kuendelea kudharau mawazo ya watanzania ambayo waliyatoa kwa ajili ya katiba mpya na kuendelea kutumia fedha za walipa kodi.

“Mimi viongozi wangu wananiamini sana, lakini pia mimi ni mpiganaji mkubwa na hivyo sipo tayari kuwasaliti wana Ukawa, kumbuka kuwa viongozi wa Ukawa wameisha toa msimamo wa kutorudi bungeni, leo iweje mimi nifanye hivyo…?
“Sitegemei wala sitarajii kurudi bungeni kuendelea na vikao haramu ambavyo vinaendelea, kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kutumia fedha za walipa kodi bila kuwa na sababu,”  alisema.
Alisema kuwa yeye ni mtetezi wa wananchi ambao ni wanyonge pamoja na umasikini wake lakini hawezi kuwasaliti wananchi kwa ajili ya vijiposho ambavyo wanapokea.
Akizungumzia kuonekana kwake katika viwanja vya bunge, alisema kuwa aliacha gari lake ambalo lilikuwa limeharibika kifaa kimojawapo.
“Baada ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti, mimi na wenzangu tulichaguliwa kuwakilisha Tanzania katika kongamano la elimu juu ya HIV na udhibiti wa matumizi ya madawa ya kulevya nchini Australia …
“Hivyo niliacha gari langu katika yadi na juzi nilitoka Dar es Saalam na basi hadi Dodoma kwa kuwa nilinunua hicho kifaa huko Dubai wakati nikirudi, nilienda bungeni kuchukua gari langu na ilikuwa usiku kama saa tatu hivi, sasa najiuliza nani aliniona naenda kusaini kama siyo propaganda ili kutuvuruga Ukawa,” alihoji Abwao.

0 comments:

Chapisha Maoni