Mh.Mwigulu
Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya
Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali
kwenye Mkono.Mh.Mwigulu
Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo
likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa
Barabara ya Iringa-Morogoro.Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo.Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla ya kumkimbiza kwenda hospitali ya WIlaya ya Mikumi.
Na.Festo Sanga.
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo kubwa
na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea
Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Roli Kubwa lililokuwa likitokea
Dsm kuelekea Barabara ya Iringa.
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya
Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa nyuma ya Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta
na Kuanguka haikuleta madhara makubwa.
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa
amekuwa akisaidia kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo
barabarani,hata kwenye ajali hii alilazimika kuhakikisha majeruhi
wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya hatua kubwa zaidi za
Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba alitumia Boksi
lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao
iliwasitoke sana Damu.
Wananchi na Madreva waliopata kusimama
kwenye ajali hiyo,Walimpongea sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna
alivyosaidia kuokoa Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi
walisikika wakiomba Viongozi wengine waige mifano hii ya Mwigulu ya
Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa sababu imekuwa ikitokea
Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi ratiba za kazi
zao.
0 comments:
Chapisha Maoni