Jeshi
la polisi nchini Brazil limesema kuwa linawashikilia watu 11 ambao
wametengeza kundi linalojihusisha na uuzaji wa tiketi za kombe la dunia
kinyume cha sheria.
Mtandao huo unadaiwa kuwa limejipatia fedha kinyume cha sheria kwa
kuuza tiketi na tayari wamefanya uhalifu huo katika viwanja vinne vya
kombe la dunia.
Baadhi ya tiketi hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya wadhamini
wakati nyingine zikiwa zimewekwa kwa ajili ya maafisa wa timu ya Brazil.
Polisi wanaamini kuwa baadhi ya tiketi zimeuzwa kwa watalii wa kigeni.
Julai 03, 2014
Taarifa,Kuhusu kundi la wahalifu linalouza tiketi za kombe la dunia kinyume cha sheria Brazil.
Posted on Alhamisi, Julai 03, 2014 by Unknown
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni