.
Msanii
wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Ndugu Haji Noorah ambaye Kimziki/Sanaa
anafahamika kwa Jina la Noraah A.K.A Baba Stylez(Starz) akizungumza na
Vyombo vya Habari kuhusiana na Mwenendo wa Afya Yake.Habari Kwanza Blog
imekutana na Msanii Noorah kujua hali ya Afya yake"Kimsingi naendeea
Vizuri kwa sasa,Nilikuwa nimelazwa Hospitali ya Kairuki(Mikocheni
Mission Hospital) kwa tatizo la Tumbo,Nimekuwa nikizumbuliwa na Tumbo
kwa Muda wa miaka 20 nikidhani ninatatizo la Vidonda vya tumbo kumbe
ndivyo Sivyo,Baada ya Vipimo vya Madaktari wamegundua ninatatizo kwenye
Utumbo wangu,hivyo wameshaanza kunifanyia Matibabu na hali yangu
imeendelea Kuimarika kadri ya siku zinavyo kwenda".Alisema Noorah.
Hit Maker wa Lugha Gongana Noraah
anaongeza "Rai yangu kwa Watanzania na Wasanii wote tuwe na tabia ya
Kufanya Uchunguzi wa Afya Zetu,Mimi nimekuwa na tatizo hili kwa Muda wa
miaka 20 nikidhani ni tatizo la kawaida tu,baada ya kupima nimegundulika
na tatizo kwenye Utumbo wangu,nashukuru Mungu sana Madaktari wamefanya
kazi kupitia Operesheni ya Tumbo,hivi sasa naendelea Vizuri".
Noorah amewashukuru sana Wasanii wote na
Watanzania wanaoendelea kumuombea na kumjulia hali yake,Hii inaonesha
ni nanma gani Wasanii tunatakiwa kitu kimoja wakati wa Shida na Raha.
Rais
wa Shirikisho la Mziki Tanzania Ndugu Addo Novemba Mwasongwe
akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya Kuwasili na Ujumbe wake
Nyumbani kwa Msanii Noorah kwaajili ya Kumjulia hali yake na kutoa
mchango wao kwaajili ya Afya ya Msanii Noorah.Rais wa Shirikisho la
Mziki Tanzania amesisitiza Umoja miongoni mwa Wasanii wakati
wote,Shirikisho linaomba Wasanii kusaidiana katika Shida na
Raha,"Tumekuaja kumuona Noorah kwasababu ni Mwanamziki Mwenzetu na
amekuwa bega kwa bega kwenye sanaa yetu,Shirikisho linatoa Rai kwa
Wasanii na Watanzania kuja kumuona Msanii mwenzao hapa Nyumbani,kumjulia
hali na hatimaye Uwe utamaduni wetu kwa Wasanii wote tunapopatwa na
Matatizo."Alisema Addo.Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Mziki Tanzania Ndugu Samwel Braiton alimaarufu
Braiton Mtz na Mmiliki wa Backyard Reckords akizungumza na Vyombo vya
Habari nyumbani kwa Msanii Noorah hii leo alipofika kwaajili ya Kumjulia
hali.Kubwa zaidi Braiton amewaomba Wasanii kujenga Utamaduni wa
Kusaidiana na Kujuliana hali,haitakuwa afya sana hadi mtu apate tatizo
kubwa sana ndipo watu waanze kujitokeza"Nawasanii Wasanii wote tuungane
katika hali yoyote na tujenge utamaduni wa kujuliana hali". Rais
wa Shirikisho la Mziki Tanzinia Ndugu Addo Novemba Mwasongwe akikabidhi
Mchango wa Fedha Taslimu Laki tano kwa Msanii Noorah hii leo walipofika
Nyumbani kwake kwaajili ya Kumjulia hali yake ya Kiafya.Ujumbe
kutoka COSOTA,Kushoto ni Philemon Kila Ofisa Msajili wa Umiliki kazi za
Wasanii,katikati Msanii Noorah na Kulia ni Ofisa kutoka COSOTA
anayeshughulikia Teknolojia na Mawasiliano.Hapa
ni Mkurugenzi wa Habari Kwanza Media/Blog Ndugu Sanga Festo akiwa
katika Picha ya pamoja na Msanii Noorah baada ya Kumtembelea Nyumbani
kwake Sinza-Darajani hii leo.
Hivi Sasa Noorah anaendelea na Matibabu
katika Hospital ya Mikocheni(kairuki) kwa mfumo wa Kliniki na anatarajia
kuhudhuria Kliniki baada ya wiki mbili kaunzia sasa.Jumla ya Gharama
zake za Matibabu hadi sasa zimefikia Milioni 2.7,Wasanii/Watanzania
mnaomba kuungana na kutoa sapoti yenu kwa ndugu Yenu na Msanii wenu
Noorah katika kipindi hiki cha Kurejesha afya yake katika hali ya
kawaida iliaendelee na majukumu ya Kila siki katika sanaa na Maisha yake
binafsi.
Picha na Habari kutoka kwa Sanga Festo wa Habari kwanza Media/blog
0 comments:
Chapisha Maoni