Text Widget

Recent Posts

Desemba 12, 2013

Jinsi kitendo cha Obama kumsalimia Castro kilivyopingwa Marekani.


cnn 1Baadhi ya Maseneta wa majimbo mbalimbali nchini Marekani wamekosoa kitendo cha Rais wa nchi hiyo
Barack Obama kupeana mkono na kiongozi wa Cuba Raul Castro wakati wa kumuaga mzee Nelson Mandela Johannesburg South Africa.


Mmoja wao ambae ni Bi Lehtinen amesema ‘wakati kiongozi wa ulimwengu huru anaposhikana mkono na kiongozi ambae ni dikteta inaonekana wazi kabisa kwamba hili ni tukio lililopangwa, Raul Castro anatumia mkono huu huu kutia saini maamuzi ya kikatili yanayokandamiza, kunyanyasa hata watu wasio na hatia’
‘Hivi tunavyozungumza Viongozi wa Upinzani Cuba wanakatwa na kuteswa kwa kupigwa bila hatia, wanafungwa gerezani na kufanyiwa mengine ya kikatili kupitia ruhusa ya mkono huohuo wa alioshikana nao Rais Obama’ – Lehtinen.
Obama JobergPamoja na kushikana mkono na Raul, Rais Obama kwenye hotuba yake aliyoitoa muda mfupi baadae alionekana kumpa madongo Raul kwa kuwaponda wanaomlilia Mzee Mandela wakati wao wenyewe wanashindwa kutekeleza yale mazuri aliyokua akiyafanya ikiwemo siasa za kistaarabu.
Obama Raul 2Wengine waliopinga kitendo cha Rais Obama kumsalimia Raul kwa kupeana mikono ni Seneta John McCain ambae amesema hiki kitendo ni sawa na kupeana mkono na Adolf Hitler na kusisitiza ‘kwa nini upeane mkono na mtu ambae bado anawashikilia Wamarekani kwenye magereza yake?’

0 comments:

Chapisha Maoni