Text Widget

Recent Posts

Novemba 11, 2013

HATIMAYE DIAMOND ATOA TAMKO LA ATAKAE MUOA KATI YA WEMA AMA PENNY

Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye.

Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya paparazi wetu Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.

Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.


“Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond.

0 comments:

Chapisha Maoni