Text Widget

Recent Posts

Septemba 23, 2014

Wananchi zaidi ya 500,000 wasajiliwa kwa ajili ya Vitambulisho vya Taifa


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ofisi ya ZANZIBAR imesajili zaidi ya wananchi 500,000 kwa ajili ya vitambulisho vya taifa.
Mamlaka hiyo imesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 82.31 ya watu zaidi ya laki 6 wanaotarajiwa kusajiliwa ifikapo mwezi OKTOBA mwaka huu ambapo wananchi zaidi ya LAKI MOJA NA ELFU 20 hawajasajiliwa kutokana na sababu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIDA Ofisi ya ZANZIBAR, VUAI MUSSA SULEIMAN ambaye alikuwa akitoa tathmini juu ya zoezi la usajili wa vitambulisho vya taifa kwa upande wa ZANZIBAR, amesema wakati wa usajili huo ofisi yake imegundua kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu suala hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni