Text Widget

Recent Posts

Septemba 23, 2014

ISRAEL yaishambulia na kuiangusha ndege ya SYRIA


ISRAEL imeishambulia na kuiangusha ndege ya kijeshi ya SYRIA katika milima ya GOLAN, ikiwa ni tukio la kwanza katika kipindi cha miaka THELATHINI.
ISRAEL imeeleza kwamba inawezekana ndege hiyo ya jeshi la SYRIA ilipita katika eneo la anga linalodhibitiwa na jeshi lake kwa bahati mbaya.
SYRIA imelielezea tukio hilo kuwa ni la makusudi.
Eneo ilikoshambuliwa ndege hiyo limekuwa likishuhudia mashambulizi baina ya wapiganaji wa kundi la AL QAEDA wanaohusishwa na kundi jingine la wapiganaji la NUSRA na wale wanaomuunga mkono Rais BASHAR AL ASSAD wa SYRIA.

0 comments:

Chapisha Maoni