Hizi ni zawadi za heshima kwa watu wa heshima |
Mbunge Mgimwa akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa darasa la saba Kiponzelo |
Baadhi ya wahitimu wa darasa la saba Kiponzelo |
Mmoja
kati ya wazee wa kijiji cha Kiponzelo akimpongeza mbunge wa jimbo la
Kalenga Godfrey Mgimwa (kulia)kwa kuwatumikia vema
…………………………………………………………………………..
Na Matukiodaima.co.tz
MBUNGE wa
jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa amepiga marufuku wazazi
wa wanafunzi waliofanya mtihani wa taifa wa darasa la saba 2014
kuwaruhusu watoto wao kwenda mijini kufanya kazi za ndani (uyaya) kwa
madai kuwa kazi hiyo ni aibu kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Iringa.
Akizungumza
katika mafahali ya darasa la saba katika shule ya msingi Kalenga na
Kiponzelo jana mbunge Mgimwa alisema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa
ukisifika kwa kutoa wafanyakazi wa ndani jambo ambalo ni aibu na
asingependa jimbo lake la kalenga kuwa katika orodha ya majimbo
yanayosifika kwa kutoa watoto wa kazi za ndani .
Mbunge
huyo alisema kuwa kwa muda ambao atakuwepo madarakani kama mbunge wa
jimbo la Kalenga atafurahi zaidi kuona wazazi wanawasomesha watoto wao
elimu ya sekondari ama elimu ya ufundi ili kuja kuwasaidia mbeleni
badala ya kuwaruhusu watoto hao kwenda mijini kutumikishwa kazi na ndani
na katika madangulo ambayo yanaweza kuwasababishia watoto hao kurudi
kijijini na maambukizi ya virusi vya UKIMWI .
” Wazazi
wa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba katika shule zote za msingi
jimbo langu la Kalenga ninaomba sana kuungana katika kulijenga jimbo la
Kalenga kwa kutowaruhusu watu wenye nia mbaya kuja kukusanya watoto wetu
na kuwapeleka mijini katika kazi za ndani na madangulo ”
Kwani
alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wazazi kutopenda kuwasomesha watoto
elimu ya sekondari na kuwaruhusu kwenda kufanya kazi ya ndani si heshima
kwa wakazi wa jimbo la Kalenga na wakazi wote wa mkoa wa Iringa bali ni
aibu kubwa ambayo kama isipo kemewa yaweza kuendelea kujenga dhana ya
kuwa mkoa wa Iringa ni kisima cha wafanyakazi wa ndani.
Mbunge
Mgimwa ambae ni katibu wa wabunge wa mkoa wa Iringa alisema kuwa umefika
wakati wa wakazi wa Iringa kuungana pamoja na kuugeuza mkoa huo kuwa ni
mkoa wa maendeleo badala ya kuwa mkoa wa kuzalisha wafanyakazi wa
ndani.
“Tukiungana
pamoja tunaweza kuufanya mkoa wa Iringa kuwa wa elimu zaidi hasa
ukizingatia mkoa wetu unaongoza kwa kuwa na vyuo vikuu vingi zaidi
kuliko mikoa mingine hivyo fursa tuliyonayo ni vema kuiendeleza kuanzia
ngazi ya chini kwa kuhakisha wanafunzi wanaomaliza shule za msingi
wanaendelea na masomo badala ya kuwaruhusu kwenda kufanya kazi za ndani
mijini”
Alisema
kuwa ni vema viongozi wa vijiji vyote vya jimbo la Kalenga kuweka
mkakati wa kuwalinda watoto hao waliomaliza darasa la saba kwa
kuhakikisha wanakwenda sekondari na wale ambao hawajabahatika
kuchaguliwa basi wanapelekwa katika vyuo vya ufundi kwa faida ya jamii
ya wana kalenga badala ya kuwaacha kwenda vijiweni na kufanya kazi za
ndani mijini.
Pia mbali
ya kuwataka wazazi kuwalinda watoto hao kutochukuliwa na watu kwenda
mijini kufanya kazi za ndani bado alitaka wale wote wenye tabia ya
kwenda vijijini kukusanya watoto kwa ajili ya kuwapeleka mijini kufanya
kazi za ndani na zile za madangulo kuachana na tabia hiyo na kuwa iwapo
watabainika basi viongozi wa vijiji ,kata na wilaya wasisite
kuwachukulia hatua kali kama njia ya kuwalinda watoto hao.
”
Tunataka mkoa wa Iringa hasa jimbo langu la kalenga kuwa mfano wa
kulinda haki za watoto na kuhakikisha dhana ya Iringa na Kalenga kuwa ni
chuo cha uyaya inafutika na kuwa ni chuo cha kuzalisha wasomi ambao
watapata kutumika katika wizara mbali mbali nchini…..leo ukiangalia
wizara mbali mbali hapa nchini wakazi wa mkoa wa Iringa waliopo ni
wachache sana ukilinganisha na wakazi wa mikoa mingine hivyo lazima mkoa
wa Iringa uje kuwa na idadi kubwa ya watumishi wa wizara mbali mbali
nchini”
Katika
mafahali hayo mbunge Mgimwa alijitolea kusaidia ujenzi wa choo cha
wanafunzi katika chule ya msingi Kalenga kwa kutoa fedha za kununua bati
zote 43 pamoja na kusaidia ujenzi wa vyoo vy matundu 18 ya wanafunzi
katika shule ya msingi Kiponzelo .
0 comments:
Chapisha Maoni