Watu
wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamiana kuwaua mume na mke na
kumjeruhi mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyeachwa na mama yake
aliyeuliwa katika tukio lililotokea kijiji cha Murvyagira wilayani Ngara
mkoani Kagera Ijumaa ya Agost 08,2014.
Kwa
mujibu wa mtoto wa marehemu amesema majambazi hao walivamia nyumbani
kwao majira ya saa 3 usiku ambapo walitumia panga na jembe kuwaua baba
na mama yake na kisha kuwapora Maharage gunia moja, Radio, Gunia la
Karanga, Mabati na Fedha vitu ambavyo hadi sasa thamani yake
haijajulikana, huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.
Aidha baadhi ya
wananchi walioongea na Blog hii, wameomba juhudi ya kuimarishwa hali ya
usalama na ulinzi wilayani Ngara izidishwe hasa wakati huu ambako
matukio ya mauaji yamezidi kujitokeza.
Mwili wa mwanaume ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa kwa kukatwa Mapanga na watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi.
Mwili
wa mwanamke ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa na majambazi hao. Mama
huyo ameacha Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyejeruhiwa na watu
hao wanaodhaniwa ni majambazi.
0 comments:
Chapisha Maoni