Text Widget

Recent Posts

Agosti 11, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA WANASAYANSI VIJANA JIJINI DAR .


1
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha na OMR 
2
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, akizungumza katika Kongamano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufungua kongamano hilo. Picha na OMR
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati akifungua Kongamano la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la tatu la Kimataifa la Mtandao wa Wanasayansi  Vijana Duniani (YES). Aidha Kongamano hilo lililoshirikisha jumla ya wajumbe zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi pia, litajadili usimamizi wa Rasilimali mbalimbali zikiwemo Mafuta na Gesi.  Picha na OMR 4 5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya sanamu la mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo. Picha na OMR
6
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akipokea zawadi ya picha ya mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto)  ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo. Picha na OMR
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  zawadi ya ramani ya Afrika, Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo. Picha na OMR 8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, baada ya ufunguzi. Picha na OMR 9

0 comments:

Chapisha Maoni