NA SYLVESTER
DAVID
MTAYARISHAJI
na msanii maarufu wa muziki nchini,Emanuel Mkono, ‘Nah Reel’amefungua studio ya
kufanyia muziki yenye lengo la
kusaidia kuboresha kazi za wasanii .
Akizungumza
na Tanzania Daima studioni kwake Cocacola, Mwenge jijini Dar es salaam,alisema amefungua
studio yake binafsi inayojulikana kwa jina la ‘The Industry’ kutokana na kukosa
muda wa kutosha wa kufanya kazi nyingi hii ni kutokana na kupokezana majukumu baina ya
watayarishaji wenzake katika studio aliyokuwa akifanya awali .
Nah Reel
ambaye amewahi kuwa mtayarishaji wa muziki katika studio mbalimbali nchini zikiwemo
Kama Kawa Record,Home Town Record,Switch Record na The Industy na kufanya
nyimbo kama,Tanzania ya Roma Mkatoriki,Wimbo Wa Taifa ya Kalla Jelemaya, Niaje
Nivipi ya Nick wa 2,Come Over ya Vanesa Mdee , Mfalme ya Mwana Fa,Ridhiwan Ya
Izzo Busness,Nyimbo zote za kundi la Weusi na Navy Kenzo na nyinginezo kibao.
“Nimeamua
kufungua studio yangu kutokana na ndoto zangu tokea zamani za kumiliki studio vilevile kuwa na muda mwingi wa
kufanya kazi zangu kutokana na mahitaji ya watu kwa muziki wangu na kusaidia
kuboresha muziki nchini”, alisema
Aliongeza
kwa kuwataka wasanii pamoja na waandaji wa muziki kuwa na sera madhubuti za kulinda kazi ili
ziwafaidishe bila kutegemea serikali.
0 comments:
Chapisha Maoni