Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuja na Fistula Ice Bucket Challenge ‘#BongoIce’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya akina mama wajawazito wenye ugonjwa wa Fistula.Hii ni kutokana na kampeni inayoendelea mitandaoni iitwayo #ALSIceBucketChallenge ambapo Vodacom Tanzania kwa kutambua kuwa kuna wanawake zaidi ya 30,000 wanaogua ugonjwa huu hapa nchini imeanzisha kampeni inayoitwa #BongoIce.
Mkurugenzi wa Vodacom, Rene Meza amekuwa wa kwanza kushiriki kampeni hii na kuwateua Naibu Waziri wa Mawasiliano January Makamba, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo Diego Gutierrez na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel ndugu Sunil Colaso kushiriki kampeni hii.
Tazama ilivyokuwa hapa chini..
0 comments:
Chapisha Maoni