NA SYLVESTER
DAVID
MSANII
chipukizi wa muziki wa Hip Hop nchini,Jafari
ahmed, ‘Jefryder’,amesema vyombo vya habari havisaidii kukuza muziki wa
wasanii wachanga na huendelea kukuza migogoro baina ya wasanii nchini.
Aliyasema
haya jana Jijini Dar es salaam alipokuwa
akizungumza na mwandishi wa habari hizi,kuwa vyombo vingi vya habari nchini hucheza
nyimbo za wasanii maarufu bila kusahau kuwa hata wao walitokea mbali
ukilinganisha na wasanii wachanga.
“Kuna wakati
ukiwa unasikiliza redio au kusoma magazeti mbalimbali, huzungumzia habari na
kupigwa nyimbo za wasanii maarufu tu wakati pia kuna wasanii wachanga,hali hii huchangia kutokukua
kwa muziki wa chipukizi,”Alisema
Jefryder
ambaye ni mjasiriamali na msanii anayetamba na wimbo wa ‘Nipe Love’
aliomshirikisha msanii Steve Rnb na Darasa, aliongeza kuwa vyombo vya habari
pia hutumika kuchochea migogoro miongoni mwa wasanii nchini na kufanya muziki
kutofika anga za kimataifa ukilinganisha na nchi jirani za Kenya na Uganda.
Pia
aliwataka mashabiki wake wawe tayari kuupokea wimbo wake mpya unaoitwa, ‘Msaliti’,
alimshirikisha mwanadada Mganda Em lee na wimbo mwingine aliomshirikisha msanii
maarufu nchini, ‘Ommy Dimpoz’.
0 comments:
Chapisha Maoni