NA SYLVESTER DAVID
MASANII maarufu wa muziki wa
Hip Hop nchini,Azma M ponda ‘Azma’, amewataka mashabiki wake wakae tayari kwa
ujio wa wimbo mpya aliomshirikisha Nakaaya Sumari ‘Nakaaya’ uitwao ‘Mvua ya
upendo’ ambao utawajia hivi karibuni.
Akizungumza na Tanzania
daima jana jijini Dar es salaam,alisema,wimbo
huo ambao ni waina yake umebeba hisia za mapenzi ya kweli.
Azma ambaye yupo katika kundi
la muziki la ‘Tamaduni’ lenye makazi yake jijini Dar es
salaam aliwahi kutamba na nyimbo kama,
Bongo Fleva inakufa,We never give up na Utata wa Katiba,alisema wimbo huo
umefanyika Jijina Arusha katika studio ya Noiz Makers.
“Wimbo wangu umebeba radha na
ujumbe muhimu katika maisha ya halisi ya mahusiano,mashabiki wangu waupoke
naamini wataupenda sana,”alisema.
Pia alisema juzi alikuwa katika ziara ya
kuzunguka mikoa 12 nchini kwa ajili ya mauzo ya albamu ya wimbo wake wa‘Love
Stories’ kutokana na mfumo duni usambazaji nchini na kufanya utafiti wa soko
lake la muziki.
0 comments:
Chapisha Maoni