Text Widget

Recent Posts

Agosti 16, 2014

HABARI PICHA: HIZI NI SHANGWE ZA SERENGRTI FIESTA BUKOBA

Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki(kushoto) ndie alikuwa Mgeni rasmi  katika Tamasha la Serengeti fiesta 2014 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Tamasha limefanyika usiku wa kuamkia leo. Viongozi mbalimbali wa Serikali, Pamoja na Wananchi mbalimbali walihudhulia kwa wingi katika Uwanja huo wa Kaitaba. katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoa Mheshimiwa Zipporah Pangani na kulia ni Bw. Denis.
Mkurugenzi wa Vipindi, Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group, Ruge Mutahaba akizungumza jambo  na kumkaribisha Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki jukwaani na kusalimiana na Wakazi wa Bukoba waliokuwa kwenye Tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2014 kwenye Uwanja wa Kaitaba

Kikundi cha Muziki cha hapa Bukoba kilichoshinda na kujinyakulia zawadi kupitia  shindano la Serengeti fiesta 2014 Supa Nyota.
Mkurugenzi wa Vipindi,Uzalishaji na Mipango wa Clouds Group, Ruge Mutahaba (wa kwanza kulia) akiwapongeza washindi na kuwapa maelekezo Msanii wa Muziki Ras Nod akiwaburudisha mashabiki wake jukwaani kwenye tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Msanii wa mjini  Bukoba, Nshomile akiimba mbele ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Kaitaba wakati wa Tamasha la Fiesta 2014, Tamasha lililofanyika kwa mara ya kwanza katika Mkoa huu wa Kagera na kushuhudiwa na Wakazi wengi wa Mji huu na Vitongoji vyake.Wadau wakifuatilia kinachoendelea kwenye Serengeti Fiesta 2014 iliyofanyika mjini Bukoba usiku wa kuamkia leoMsanii mkongwe wa nyimbo za asili za Kihaya, Saida Karoli  akiwa na Kundi lake zima wakipagawisha Wakazi wa Bukoba usiku wa kuamkia leo kwenye Tamasha la Fiesta 2014.Saida Karoli akicharaza ngoma tatu kwa mpigo na kuwashangaza Mashabiki wake.Hakika ilikuwa ni Sheeeeda!!! Hii ni Historia katika mji wa Bukoba.Willy O. Rutta akionesha Shangwe ya nguvu kwenye Fiesta 2014 iliyofanyika siku ya ijumaa mjini Bukoba
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Recho akifanya ya kwake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 lililofanyika mjini Bukoba.Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Jux nae akwapagawisha mashabiki wake mjini BukobaLinah na waimbaji wake wakifanya yao kwenye Usiku wa FiestaLinah akipawawisha Mashabiki wake 
Barnabas akitoa burudani ya nguvu kwenye stage ya Serengeti Fiesta 2014 mjini Bukoba.Mr. Blue akitoa burudani ya nguvu kwenye tamasha hiloMsanii chipukizi BK Sande akiimba mbele ya mashabiki wake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 lililofanyika mjini Bukoba.
Ilikuwa ni Shidaaaaaaaa!!!!!!!!!
Simu nazo zikawa Viganjani juu kwa juu!! Kuamsha Fiesta!!! Upendo nao ukisambazwa kitaratiiibu!

0 comments:

Chapisha Maoni