NA SYLVESTER DAVID
TIMU za soka za Mbile FC na
Mshale FC leo zitashuka dimbani katika mechi ya fainali ya kuwania ubingwa wa
michuano ya Kombe la Mshikamano itakayopigwa uwanja wa Kinnes, Urafiki, jijini
Dar es Salaam.
Akizungumzia mechi hiyo jana,
Rama Risasi ‘No Fear’ ambaye ni kocha wa
Mshale FC, alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na kila moja kukamia
ushindi kutwaa ubingwa.
Alisema kama vijana wake
watacheza vizuri kama mechi zilizopita tangu kuanza kwa michuano hiyo Juni 29
katika hana hofu na ubingwa.
Alisema michuano hiyo
iliyoshirikisha jumla ya timu 10, mechi za robo fainali zilipigwa katika viwanja
vya Las Vegas, Mabibo na kuanzia nusu fainali zikahamia Uwanja wa Engo, Kinesi
Urafiki.
“Kesho (leo) sisi Mshale FC tutacheza
mechi ya fainali dhidi Mbile FC, nawasihi wapenzi na mashabiki wetu waje
kutushangilia, tumejipanga vizuri kuibuka mabingwa,” alisema Risasi
Alisema kwa upande wao
wamejiandaa vizuri kwani vijana wake wamekuwa wakicheza soka ya uhakika tangu kuanza
kwa michuano hiyo ambapo hadi kufikia fainali ya leo, timu yake haijapoteza
mechi.
Kuhusu zawadi, Risasi alisema
bingwa atapata Kombe na jozi 30 za jezi; mshindi wa pili ataondoka na mbuzi
huku kukiwa hakuna zawadi kwa mshindi wa tatu.
Aliongeza kuwa, lengo la michuano
hiyo ni kuibua na kukuza vipaji vya vijana, kukuza umoja miongoni mwa
wachezaji, kuboresha afya na kuamsha ari ya vijana kupenda michezo.
Risasi alisema mgeni rasmi
katika mechi ya leo, atakuwa ni
Seleman Masawe.
Akielezea upande wa timu yake ya Mshale
alisema,wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuchukua kikombe hicho kwani wachezaji
wote wako vizuri kiafya hivyo mashabiki wategemee soka safi kutoka kwenye timu
yake lakini haibezi timu pinzani na kueleza kuwa mpira ni dakika 90.
0 comments:
Chapisha Maoni