Fundi: Angel Di Maria aliichezea Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid katika mechi ya Super Cup
MANCHESTER United wanakaribia kukamilisha usajili ghali wa Muargentina, Angel Di Maria kwa paundi milioni 60.
Uhamisho huo ukikamilika utavunja rekodi ya klabu hiyo katika usajili.
United
wamekuwa wakifuatilia dili la nyota huyo wa Real Madrid kwa muda mrefu
na inafahamika kuwa wametoa ofa ya mshahara wa paundi laki mbili kwa
wiki.
Kiwango
cha juu: Di Maria anatarajia kujiunga na Manchester United kwa ada ya
uhamisho ya paundi milioni 60 na mshahara wa paundi laki mbili kwa
wiki.
Kifaa cha ukweli: Gary Neville anaamini kuwa Di Maria ndio aina ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa na Manchester United
0 comments:
Chapisha Maoni