Cecilia Hamis (kulia) akiwa na mume wake (mtuhumiwa) Hamis Juma.
LILE sakata
la mume aliyetajwa kwa jina la Hamis Juma (pichani akiwa na mkewe),
mkazi wa Majhe Mji Mpya, Ilala jijini Dar kudaiwa na mkewe, Cecilia
Hamis kwamba amempa mimba mbwa yameibuka mapya, Uwazi limeyanyaka.
Ijumaa
iliyopita, Uwazi lilifika kwenye ofisi za Taasisi ya Kutetea Haki za
Wanyama ambapo mmoja wa maofisa aliyedai si msemaji maalum, alisema wapo
katika mchakato wa kufuatilia madai ya mke wa mtuhumiwa huyo kisha
kumpandisha mahakamani kujibu mashitaka ya kumdhalilisha mnyama huyo.
Mbwa anayedaiwa kupewa mimba na Bw. Hamis Juma.
“Sisi
ishu yetu si kufuatilia kama kweli amempa mimba bali ni kujiridhisha
kama kweli yule mzee ametembea na mbwa hilo linatosha kabisa kumfikisha
kortini,” alisema afisa huyo na kuomba jina lake lisichapishwe gazetini. WAGOMA MBWA KUUAWA
Jingine
jipya lililotua Uwazi linadai kuwa, baadhi ya majirani wa nyumbani kwa
Hamis wamegoma mbwa huyo kuuawa baada ya wengine kutaka kufanya hivyo
wakisema hali hiyo itaweza kusababisha mdaiwa huyo kufanya matukio
mengine nje ya nyumba yake.
MENGINE TENA
Katika hatua nyingine, Uwazi limebaini kuwa, kumbe mwanaume huyo ana
sakata lingine ambapo ana kesi kwenye Mahakama ya Mwanzo Ukonga jijini
Dar akikabiliwa na tuhuma za kumfanyia fujo jirani yake.
Kwa mujibu wa taarifa za kimahakama, ilidaiwa kuwa Hamis alifika
nyumbani kwa Alanus Haule ambaye ni jirani yake saa saba usiku wa siku
ya tukio akiwa na silaha za kienyeji na chepe akiwa amelewa na kuanza
kumtolea maneno ya vitisho huku akijua ni kosa kisheria chini ya kifungu
cha sheria 89 (1) B CAP 16.
Kesi hiyo yenye No 873/2014 ambayo inasikilizwa na Hakimu Mwandamizi,
Raia Omary kwa mara ya mwisho ilisikilizwa Julai 3, mwaka huu na
kuahirishwa hadi Septemba 11, mwaka huu na yuko nje kwa dhamana.
Habari hii kuhusu Hamis Juma kudaiwa kumpa mimba mbwa, kwa mara ya kwanza.
0 comments:
Chapisha Maoni