Text Widget

Recent Posts

Machi 31, 2014

TAZAMA , PICHA ZA MAFURIKO YALIYOTOKEA LINDI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WANNE



DSC_0413DARAJA la MTAMA Llilokatika Tarehe 26/3/2014 na kuzuia mawasiliano ya barabara kati ya lindi na newala kwenda Tandahimba mkoani Mtwara.DSC_0367Baadhi ya abiria walionasa kufuatia kukatika kwa daraja Nyangao wilayani Lindi kutokana na Mvua zinazoendelea
DSC_0377Kamati ya Ulinzi na Usalama ilkiongozwa na mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Lind, Ludovick Mwananzila ilipofika eneo la Nyangao kukagua athari za Mafuriko hayo.DSC_0103Mmoja wa abiria aliekwama baada ya kukatika kwa daraja la Nyangao linalounganisha barabara ya lindi na masasi kwenda Nachingwea na Tunduru akijaribu kuvuka mara baada ya kutengeneza njia ya muda kunusuru abiria kutokana na mafuriko yaliyotokea Tarehe 26/3/2014.DSC_0198Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila akiithibitisha njia ya muda mara baada ya kukatika kwa daraja la mto Nyangao lililokatika jana, Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga waliofika kukagua athari zilizojitokezaDSC_0316Baadhi ya abiria wakivuka katika daraja la Nyangao Lindi picha na Abdulaziz Lindi

Na. Abdulaziz Video, Lindi
 
Mafuriko yaua na kusitisha usafiri Lindi Masasi,Ruangwa na Nachingwea ikiwemo Newala na Tandahimba Mkoani Mtwara
 
Watu Wanne wamefariki dunia katika wilaya ya Lindi kutokana na mvua zilizonyesha usiku wa Tarehe 26 na 27 /3/2014 na kusababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Lindi, Nachingwea na Ruangwa Mkoani Lindi

Sambamba na mvua hizo licha ya kupoteza maisha ya watu hao na wengine kujeruhiwa pia Imesitisha huduma za usafiri kati ya Lindi, Masasi, Nachingwea, Ruangwa na Newala kufuatia kukatika kwa madaraja ya Mtama na Nyangao pamoja na makazi ya wananchi wanaoishi pembezoni kulikosababishwa na kufurika kwa mto Lukuledi.
 
Akiongea na globu hii mara baada ya kukagua athari hizo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila alieleza kuwa Tayari Wakala wa barabara Mkoa wa Lindi inafanya jitihada za haraka kuweka njia ya Muda ili kuokoa wananchi wengi waliokwama katika maeneo hayo ili kupunguza msongamano uliopo Sambamba hilo Mwananzila alitoa wito kwa baadhi ya wananchi waliopo maeneo yaliyokumbwa na maafa hayo kutoruhusu watoto wao kucheza katika mto huo kutokana na ongezeko kubwa la maji.
 
Aidha Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi aliwahakikishia usalama abiria wote waliokutwa na maafa hayo kuwa Jeshi la polisi limejipanga kutoa ulinzi wakati wote katika maeneo hayo huku akitoa agizo kwa wenye mabasi ya Abiria kutofanya safari hadi kutakapokamilika kwa maeneo hayo ili kupunguza idadi kubwa ya wasafiri.
 
Kukatika kwa madaraja hayo tayari kumesitisha Usafiri kwa wanaotoka Mkoa wa Lindi kwenda wilaya za Masasi, Nachingwea, Tunduru, Ruangwa, Liwale, Nanyumbu, Newala

0 comments:

Chapisha Maoni