Mzee Small akiwa nyumbani kwake Tabata,pamoja na familia yake leo hii.
Akizungumza na Paparazi wetu aliyemtembelea nyumbani kwake Tabata Mawenzi leo asubuhi, Small amesema alipatwa na mshituko baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu wanasambaza taarifa kuwa amefariki dunia, na kumlaani mtu aliyosambaza taarifa hizo za uongo.
“Kwanza nawashukuru (Watanzania) na nawaheshimu kunipigia simu na kumtafuta mchawi, maana yake nyinyi ndiyo mumemvumbua mchawi,nawashukuru Radio zote,Tv zote nazishukuru mimi mzima bado nipo hai” Alisema Mzee huyo mcheshi.
“Kwanza mke wangu alishituka alafu mimi mwenyewe nilikuwa nimelala, lakini kwakweli mimi nilijisikia vibaya, namalaani huyo mtu,namlaani kwanzia leo mpaka kiama na mwenyezi mungu atamuona na kumsikia” Alisema Mzee Small.
Naye mke wa Mzee Small amesema kwa upande wake ameathirika kwa kiasi fulani kwakuwa yeye ni muuguzi mkuu, alihitaji kuulizwa maendeleo ya Mzee Small kabla ya kutangaza taarifa za uongo.
“Mimi ni mke wa Mzee Small kwakweli kwa tukio lililotokea limeniumiza sana kwasababu mimi ndiyo muuguzaji mkuu wa huyu bwana,niko nae inakuwa vigumu jambo kama hili linapotokea wakati mimi sijui chochote, kwakweli limeniumiza.
Nawaomba Watanzania tufike mahala tuangalie, tusianze kusambaza vitu ambavyo hatuka ukweli navyo” Alisema mke wa Small.
Tazama hapa video.
0 comments:
Chapisha Maoni