Text Widget

Recent Posts

Desemba 12, 2013

SOMA HAPA ZAIDI,"MAIMATHA WA JESSE ATAMBA KUWA VIKWAZO VINAMBEBA".

MTANGAZAJI maarufu nchini, Maimatha Jesse amesema vikwazo anavyokutana navyo katika kazi zake ndivyo vinavyomfanya afanikiwe katika mambo yake ambayo amedhamiria kuyafanya.
Maimatha alisema anakumbana na vikwazo vingi katika kazi zake mbalimbali wakiwemo baadhi ya watu ambao huamua kumwangusha kwa makusudi ili tu asifikie kile alichokusudia kukifanya.
“Unajua mimi kazi zangu nyingi huwa ninazifanya kwa kujiajiri zaidi kupitia kampuni yangu ya Manywele Entertainment, lakini huku ninakotembelea nakumbana na changamoto nyingi ambazo zinanikatisha tamaa sana,’’ alisema.
“Hata hivyo nashukuru Mungu kwani hata siku moja sijawahi kutetereka kutokana na vikwazo mbalimbali vyenye nia ya kunikwamisha,” alisema.
Maimatha kupitia kampuni yake ya Manywele Entertainment hivi sasa amehitimisha mashindano yake ya Vigori wa Extra Bongo 2013.

0 comments:

Chapisha Maoni