Ile collabo iliyozaa ngoma kali ‘Nidanganye’ mwaka 2012 kati ya Shetta na Diamond Platinumz inajirudia tena mwishoni mwa mwaka huu ambapo ngoma ya wakali hawa itasikika hewani kabla ya kuumaliza mwaka huu (2013).
Shettta amesema kuwa tayari ameshafanya ngoma nyingine na Diamond Platinumz inayoitwa Mama Qayllah na umetayarishwa na Shedy Clever wa Burn Records.
“Kwanza kabla ya yote ningependa kutoa shukrani za dhati kwa mashabiki wangu kwa kuipokea vizuri video ya wimbo wangu 'Sina Imani',kwa sasa nipo katika maandalizi ya wimbo wangu mwingine mpya kabisa humo ndani nipo mimi pamoja na Diamond,wimbo unaitwa Mama Qayllah. Bado upo katika hatua za mwisho za kufanyiwa mixing na Sheddy Clever wa Burn Records.” Sheddy Clever ameeleza.
Shetta ama Baba Qayllah kama anavyopendwa kuitwa amesema huo utakuwa wimbo wake wa mwisho wa kufungia mwaka 2013.
0 comments:
Chapisha Maoni