Waandaji wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search, wamesema mshindi wa mwaka huu ambaye ataibuka na kitita cha shilingi milioni 50, atasimamiwa na uongozi wa shindano hilo ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika pia katika kuendeleza maisha yake ya muziki na sio kuzitumia kwa matakwa binafsi.
Mwanzilishi wa show hiyo ambaye pia ni jaji mkuu, Rita Paulsen aka Madam Rita, amesema wameamua kufanya hivyo kwakuwa washindi wamekuwa wakizitumia fedha wanazopata kwa mambo mengine na kusahau muziki.
Ameongeza kuwa wameamua kufanya hivyo kuondoa lawama za watu kuwa washindi hupotea mapema.
“Tumegundua kwamba wasanii hawawezi kutumia hizo hela kujijenga. Wanaweza kutumia kwa vitu vingi ambavyo ni mahitaji pia sijui nyumba, gari,” amewaambia waandishi wa habari leo.
“Management company inaleta proposal, tunatengeneza video kadhaa, tunatengeneza promotion ya wimbo wako. Kutakuwa na mwanasheria na yeye mwenyewe anaauthorise ile hela inaenda kufanya hivyo vitu.”
Fainali ya shindano hilo itafanyika November 30, jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni