Text Widget

Recent Posts

Novemba 14, 2013

NDOA YA JOHARI KUFUNGWA NCHI MBILI

Juzi tuliweka habari hapa  kuwa actress maarufu Bongo Movies Blandina Chagula(Johari) amepata na amekwenda 
Canada kumfuata mpenzi wake raia wa nchi hiyo na pia kutambulishwa ukweni. Habari mpya ni kuwa baada ya kutambulishwa mipango ya ndoa kati ya johari na mzungu huyo itafanyika ili wawili hao waishi kama mke na mume baada ya mzungu huyo kuwa hoi bin taabani kwa penzi la Johari aliyejaaliwa kipaji cha kuigiza. Habari za mipango hiyo ya ndoa zimetolewa na Irene Uwoya alipozungumza na Bongo5 kwa kusema "akitambulishwa kitakachofuata ni ndoa, na kwa jinsi tulivyojadiliana watafanya ndoa mbili moja hapa(Tanzania) na nyingine Canada ili na sisi tulio Dar es salaam tusherehekee ndoa yake kwasababu kama unavyojua ndugu zake, marafiki na watanzania kwa ujumla wanahitaji kuhudhuria ndoa hiyo" 
Uwoya ambaye nae aliolewa na raia wa Rwanda Hamad Ndikumana kwa ndoa ya gharama na mwishowe ndoa hiyo kuwa chali aliendelea kwa kusema "Juzi niliandika kauli ya kumtaka atulie akiwa Canada, sio kwamba Johari hajatulia unajua Johari ni mtu wangu wa karibu kwa hiyo nilikuwa namwambia asipeleke uswahili Canada sio kwa nia mbaya"

0 comments:

Chapisha Maoni