Bi Grace Mugabe Kulia akiandamana na mumewe rais Robert Mugabe.
Alipewa shahada hiyo na chuo kikuu cha Zimbabwe mwezi uliopita.Lakini kumekuwa na lalama kuhusu mda aliyochukua katika chuo hicho kusomea shahada hiyo,huku baadhi ya duru zikiarifu kuwa alichukua miezi miwili pekee na sasa wanafunzi wanataka swala hilo kuchunguzwa.
Hata hivyo chuo hicho hakijatoa tamko lolote kuhusu mgogoro huo.
''Hatua hiyo inaathiri uadilifu wa kitaalam'', bwana Hove aliiambia BBC.
Bi Grace Mugabe kulia.
Shahada aliyopewa si ile ya heshima bali ni ya kusomea taaluma fulani,alisema mwandishi huyo.
Hove aliyehitimu kutoka chuo hicho cha Zimbabwe amesema kuwa alimwandikia Naibu Chansela wa chuo hicho akimtaka kuelezea hatua hiyo.
Katika barua aliomwandikia mkuu huyo, Hove amesema kuwa chuo hicho kimepoteza heshima yake kwa kuwa shahada za chuo hicho sasa hazina maana.
Matamshi yake yanajiri huku muungano wa wanafunzi wa taifa hilo ukiandaa kuwasilisha kesi mahakamani siku ya Alhamisi ukitaka chuo hicho cha Zimbabwe kutoa maelezo kuhusu vile mke huyo wa rais alivyopata shahada hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni