Ndanda FC inaongoza ligi kuu hadi nakufikia sasa kabla ya mchezo wa
Simba SC na Coastal Union jioni ya leo katika uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Ndanda ilichomoza na ushindi wa kuvutia katika uwanja wa
Kambarage, Shinyanga dhidi ya wenyeji Stand United ambao walikubali
kichapo cha mabao 4-1. Mabingwa watetezi Azam FC walianza vizuri baada
ya kuishinda kwa mara ya kwanza Polisi Morogoro katika ligi kuu. Kabla
ya kichapo cha mabao 3-1 hapo jana, timu hizi mbili hazikuwa zimefungana
katika michezo miwili ya miaka ya nyuma.
Yanga walianza na kichapo ‘ hevi’ katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro,
timu kama Mbeya City ilijikuta ikilazimishwa suhulu tasa na JKT Ruvu
katika uwanja wa Sokoine. Simba itacheza na Coastal Union katika mchezo
wa mwisho wa mzunguko wa kwanza na wanaweza kujikuta wakipoteza mchezo
huo kama mwalimu hatapanga timu yake katika usawa.
Namna gani kocha Patrick Phiri anaweza kupata ubora wa Paul Kiongera,
Emmanuel Okwi, Amis Tambwe, Ramadhani Singano na Shaaban Kisiga taakwa
kuwapanga pamoja, hilo ni jambo linalotakiwa na wapenzi wa timu hiyo
kuona mastaa wao wakigezi wakiongoza safu ya mashambulizi wakisaidiwa na
viungo wazawa wenye vipaji. Kama Phiri ataamua kuanza na wachezaji hao
watano kwa wakati mmoja, atachapwa kwa kuwa timu itakosa ‘ balansi’.
Coastal inacheza msimu wan ne mfululizo wa ligi kuu licha ya kumaliza
katika nafasi ya tisa msimu uliopita timu hiyo ilifanikiwa kuifunga
Simba katika uwanja wa Taifa katika mchezo wa mzunguko wa pili na
kulazimisha suluhu katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa
kwanza.Rama Salim mshambuli wa Kimataifa wa Kenya amesajiliwa ili
kufunga mabao kama alivyokuwa akifanya katika timu ya Gor Mahia. Coastal
itamkosa mshambulizi wake Daniel Lyanga ambaye amekwenda kufanya
majaribio katika klabu ya DCM Motema Pembe ya DRC, lakini ina uhakika wa
kufunga katika mchezo wa leo kulingana na wachezaji waliopo.
Ike Bright Obinna, Hussein Sued, Tumba Sued, wote hao wamesajiliwa
kutoka Ashanti United iliyoshuka daraja, Itubu Imbem mshambulizi
mwingine hatari kutoka Gor Mahia ya Kenya pia amesajiliwa kuongeza nguvu
katika timu hiyo ambayo imejipanga kufuta matokeo mabaya ya msimu
uliopita.
Phiri atafanya makosa akiwapanga wachezaji hao watano kwa wakati
mmoja, miongoni mwao hakuna mkabaji ambaye yupo tayari kusumbuka
kutafuta mpira ili kuisaidia timu. Miraj Adam, Issa Rashid, Joram
Mvegeke na Joseph Owino ni safu ya ulinzi ambayo inaweza kuanza katika
mchezo wa leo ila itakuwa vizuri zaidi wachezaji hao wa nyuma wakilindwa
na viungo wawili wa ulinzi na si mmoja. Pierre Kwizera anataraji
kucheza na Kisiga katikati ya uwanja, ili kuleta usawa Phiri anaweza
kumchezesha Amri Kiemba na kukubali kumuweka nje mmoja wa mastaa wake
wanne wa safu ya mbele.
0 comments:
Chapisha Maoni