Chege,
Temba, Aslay pamoja na kundi zima la Mkubwa na Wanawe Jumatano hii
walitembelea katika wodi ya watoto ya hospitali ya Temeke jijini Dar es
Salaam na kutoa misaada mbalimbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari Said Fela alisema wanajisikia vizuri kutoa
msaada kama huo kwakuwa na wao ni wagonjwa wa baadaye.
“Tumeamua
kuanza na watoto maana mimi ni mzazi na hata mke wangu anajifunguliaga
hapa pia mimi nilikuwa mtoto na katika show yetu pengine wazazi waliopo
hapa walipenda kufika lakini kutokana na kuuguza wakashindwa kufika. Na
hii hatutofanya wilaya hii tu tukipata kingine kidogo basi tutapeleka na
kwingine na hii isiwe sisi tumefunga milango wajitokeze na wengine
kusaidia,” alisema.
Temba akiwa wodi ya watoto
Aslay akiwa na wenzake
Chege
(PICHA BONGO5)
0 comments:
Chapisha Maoni