Kufuatia vurugu zilizoibuka ukumbini alfajiri ya Jumapili iliyopita
baada ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kucheleweshwa kupanda
stejini kwenye Ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart,
Ujerumani, mwanamuziki huyo anadaiwa kupigwa marufuku kutia maguu nchini
humo.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
SHUHUDA WETU
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini
mjini humo, ambacho pia kilikuwepo ukumbini wakati vurugu zilipoibuka,
uchunguzi wa awali umeonesha kwamba, gharama ya vitu vilivyoharibiwa
inakadiriwa kuwa zaidi ya Euro 128,322 sawa na Sh. milioni 280.
Viti
vya ukumbi wa Sindelfingen uliopo Mji wa Stuttgart, Ujerumani
vilivyoharibiwa na mashabiki waliopoteza uvumilivu kusubiri shoo ya
Diamond Platinum.
“Tukio la vurugu za Diamond limeripotiwa kwenye magazeti tofauti
mjini hapa lakini kubwa ni hasira ambayo mashabiki wa Diamond
wameionesha waziwazi.
“Kwa mfano Gazeti la Stuttgarter la leo (Jumatatu) la mjini hapa limeandika:
Gari la polisi likiwasili eneo la tukio kutoa Msaada.
‘MASHABIKI WANA HASIRA NA DIAMOND’.
Kwenye habari zao waliwahoji watu waliofurika ukumbini hapo.
“Wengi walikuwa wakilalamika kwamba walikata tiketi mapema kwa euro 25
(zaidi ya Sh. elfu 55) kwa kichwa. Yaani kuanzia saa 4:00 watu walikuwa
tayari wanamsubiri Diamond.
MUDA WAYOYOMA
“Kuna muda DJ alitangaza kwamba
angepanda stejini kuanzia saa 6:00 usiku hivyo watu wakapunguza hasira.
Cha ajabu saa saba ilikatika, nane ikapita, tisa ndipo mtiti ukaanza.
Mashabiki wakilizingira gari la Diamond.
“Sasa hebu fikiria mtu umetoa buku 55 yako halafu hadi saa tisa usiku
mtu haonekani! Hapo ndipo tatizo lilipoanzia!” yamesomeka hivyo
magazeti ya hapa.Ilisemekana kwamba ilipofika saa 10:00 alfajiri ndipo
Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake, raia wa Nigeria anayejiita
Kamabritts.
CHUPA ZARUSHWA
Mashabiki walipoona kuwa
hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki
huyo na promota wake.Ilidaiwa kwamba kilichowakera zaidi mashabiki hao
ni vyombo vibovu vilivyofungwa ukumbini humo kitu ambacho kiliwafanya
kuvunjavunja viti, meza, jukwaa na vyombo vya muziki kisha kusababisha
watu kujeruhiwa na hasara kubwa ya mamilioni ya shilingi.
Mapolisi wakilinda gari la diamond dhidi ya mshabiki waliokuwa na gadhabu.
MAJERUHI WAONGEZEKA
Baadhi ya vyombo vya habari
mjini humo, juzi (Jumatatu) viliripoti kuongezeka kwa majeruhi wakiwemo
MaDJ wawili ambao hali zao bado ni tete hospitalini kwa sasa.
Katika
vurugu hizo, DJ mwanamke aliyetajwa kwa jina la DJ Flor alizimia hivyo
akakimbizwa hospitalini huku mashabiki wakimpa kipigo DJ Drazee.
KAULI YA POLISI
Polisi eneo la Sindelfingen,
Stuttgart nchini Ujerumani walisema tukio hilo ni la aibu hivyo
uchunguzi wa kina unaendelea ambapo promota huyo na Diamond watalazimika
kulipa vitu hivyo na kwamba hawatawaruhusu kufanya tena shoo eneo hilo
na kwingineko nchini humo.
Magari ya wagonjwa yakiwa tayari kuhudumia majeruhi eneo la tukio.
Posted in
|
0 comments:
Chapisha Maoni