BAADA ya mechi kali kati ya wabunge mashabiki wa Simba na wa Yanga kufanyika jana katika Tamasha la Matumaini lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, waheshimiwa hao wamekutana katika Hoteli ya Atriums, iliyopo maeneo ya Afrika Sana, Dar na viongozi wa Global Publishers na kupongezana huku wakipata kifungua kinywa pamoja.
Kwenye hafla hiyo fupi, waheshimiwa wabunge walijichanganya pamoja na uongozi mzima wa Kampuni ya Global Publishers ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Matumaini ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Eric Shigongo, Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, Mhariri kiongozi wa magazeti pendwa, Oscar Ndauka na baadhi ya wahariri.
HABARI/PICHA: ERICK EVARIST GPL
0 comments:
Chapisha Maoni