Jokate Mwengelo juzikati aliamua kujizamisha rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kupanda kwa mara ya kwanza katika Jukwaa la Serengeti Fiesta 2014, akiwa na madensa wake.
Mwanamitindo maarufu ambaye aliwika na lebo ya Kidoti, Jokate Mwengelo.
Ishu hiyo
ilitokea usiku wa kuamkia Agosti 10 mwaka huu ndani ya uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza, ambapo Jokate ‘aliwa-suprise’ mashabiki akiwa
anajiamini akiimba na kutawala steji.Kwa muda wote akiwa jukwaani,
mwanamitindo huyo alicheza staili sambamba na wanenguaji wake pasipo
kupotea hata mara moja kama vile alianza zamani kuimba.
“Nina
kipaji cha kuimba, na ndiyo maana nimekuwa nikiimba kanisani siku zote,
muziki naupenda sema mwanzo nilishindwa kwenda na mambo mawili kwa
wakati mmoja, ila sasa ndiyo nimezindua rasmi harakati za muziki na siku
chache zijazo nitaachia video ya wimbo wangu nilioimba leo,” alisema
Jokate.
0 comments:
Chapisha Maoni