Stori: Mayasa Mariwata na Denis Mtima
Ni tatizo! Sexy lady wa Bongo Fleva, Winfrida Josephat ‘Recho’ ametia
fora baada ya kutinga kipensi
kilichoonesha sawia maungo yake nyeti.
Ishu hiyo ya aibu ilijiri kwenye Ukumbi wa Sun Ciro uliopo Ubungo,
Dar ambapo kulikuwa na kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Chuo cha
Ustawi wa Jamii kilichopo Dar huku Recho akiwa mtumbuizaji.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wetu, Recho alipanda kwa steji kupiga shoo akiwa
ametinga kivazi hicho ambacho kilikuwa ni sawa na ‘kufuli’ hivyo kuibua
gumzo kwenye shindano hilo ambalo aliyeibuka kidedea ni Junis Ndalima.
Baadhi ya wanachuo wa Ustawi walionesha kushangazwa na tukio huku wakiweka wazi kuwa msanii huyo ni tatizo.
Ijumaa Wikienda lilipomfuata kutaka kujua kulikoni ‘kutokelezea’ mbele za watu na kipisi hicho cha kipensi hakuwa na jibu.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
Mei 18, 2014
TAZAMA MAVAZI YA HATARIII KWENYE SHOW YARECHO NI TATIZO!
Posted on Jumapili, Mei 18, 2014 by Unknown
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni