Mei 18, 2014
Soma na hili, Cristiano Ronaldo awafunika Messi na Diego Costa – atwaa tuzo ya PICHICHI
Posted on Jumapili, Mei 18, 2014 by Unknown
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekuwa mfungaji bora na kutwaa tuzo ya PICHICHI ambayo hutolewa kwa mwanasoka anayekuwa kafunga magoli kwenye msimu mmoja wa La liga.
Ronaldo amemaliza msimu akiwa na magoli 30 baada ya kucheza 31 na kufanikiwa kuwazidi Diego Costa na Lionel Messi waliokuwa wakimfuatia kwa karibu. Pia Ronaldo amefungana kwa magoli na Luis Suarez katika kugombea tuzo ya kiatu cha dhahabu kinachotolewa kwa mfungaji bora wa ligi za ulaya.
Cristiano Ronaldo pia ni mfungaji bora wa michuano ya UEFA Champions League ambapo mpaka sasa ana magoli 16 huku bado akisubiri kucheza fainali dhidi ya Atletico Jumamosi ijayo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni