Hili pia ni tatizo la ugumba kwa mwanaume. Mbegu za kiume hupatikana katika manii au majimaji yanayotoka kwa mwanaume unapomaliza tendo la ndoa. Si kila mwanaume anayefanya tendo la ndoa vizuri au anatoa manii kwamba hana tatizo. Unaweza kuwa vizuri kumbe huna mbegu za kiume au mbegu zako hazina ubora wa kurutubisha yai la mwanamke.
Mbegu za kiume ni ndogo sana na hazionekani kwa macho hadi kwa vifaa maalum vya maabara.
Maumbile ya mbegu za kiume zina kichwa, mwili na mkia na huogelea kwenye manii na huwa na mwendo wa kasi sana.
Mwanaume hutoa kiasi cha mbegu kati ya milioni ishirini hadi milioni mia tatu na hamsini kila anapotoa manii zenye ujazo wa milimita mbili na nusu hadi tatu na nusu.
Manii yenye ubora huwa nzito kiasi na huvutika kama kamasi na zikikaa kwa muda kidogo huyeyuka.
Matatizo yanayotokea
Matatizo ya mbegu za kiume kushindwa kurutubisha yai yapo mengi, mbegu zinaweza kukosa mwendo kasi zikawa goigoi, badala ya kwenda mbele zikaenda kinyumenyume au upandeupande, nyingine hazina mikia au vichwa vimekatika na nyingine zina mikia miwili badala ya mmoja.
Mwanaume anayetoa mbegu za kiume chini ya milioni ishirini haweza kumpa mwanamke mimba. Kiwango cha manii kinachotakiwa kutoka na kubeba mbegu kisiwe chini ya milimita mbili na nusu na kisizidi tatu na nusu, kinyume cha hapo mbegu haziwezi kuwa na ubora.
Chanzo cha tatizo
Maambukizi ya mara kwa mara katika viungo vya uzazi vya mwanaume huchangia kwa kiasi kikubwa.
Mfano, Yutiai za mara kwa mara kwa mwanaume, maumivu ya mara kwa mara ya korodani, kufanya kazi katika mazingira ya joto kali, kuumia korodani ni miongoni mwa matizo yanayoathiri uzazi kwa mwanaume kwa kiasi kikubwa.
Ukosefu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa, kwani utashindwa kutoa manii.
Matumizi ya dawa za kulevya mfano uvutaji bangi, mirungi, Heroin, Coacaine na nyingine huathiri uzazi au huuwa kabisa uzazi kwa mwanaume.
Uvutaji sigara na ulevi wa kupindukia pia huathiri uzazi hasa unywaji wa pombe kali.
Maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ‘Mumps’ pia huharibu korodani na kuua uzazi hasa unapopata ugonjwa huu katika umri wa kuoa na unatafuta mtoto utakuwa unafanya tendo la ndoa vizuri, unatoa manii lakini mimba hakuna. Hii ni kutokana na kutokuwa na mbegu za uzazi.
Dalili za tatizo
Hakuna dalili za wazi kwamba mwanaume mwenye tatizo la uzazi yupo hivi, bali dalili za moja kwa moja kwamba una tatizo la uzazi ni kutokuwa na nguvu kabisa za kufanya tendo la ndoa, kushindwa kabisa kutoa manii wakati wa tendo, kutoa manii mepesi sana kama maji, kutokuwa na korodani, unatakiwa uwe na korodani mbili, kama unayo moja basi ni vema ukapima mbegu zako ili kuthibitisha kama una uwezo wa kuzaa.
Uchunguzi
Hufanyika kwenye kliniki za matatizo ya uzazi, katika hospitali za wilaya na mikoa.
Vipimo vya manii ili kuangalia kama unazo mbegu za kiume, je mbegu hizo zina ubora?
Zina kasi ya kutosha? Zina kiwango kizuri? Pia zitaangaliwa kama hakuna maambukizi wala kasoro. Pia korodani itachunguzwa kama kuna tatizo kwa ndani.
0 comments:
Chapisha Maoni