Sasa kutokana na hali hiyo leo jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam wameitisha kikao cha makamanda wote wa jiji hili kisha baadae kuitwa waandishi wa habari kwa ajili ya matukio ambayo yamewahi kufanywa na vijana hao,kwa sasa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanya msako na doria katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti makundi ya uhalifu wa aina mbalimbali.
Makundi hayo ni pamoja na vijana wahuni wasio na kazi maalu maarufu kwa jina la MBWA MWITU au PANYA ROAD.Maeneo yote ambayo yametajwa kuonekana vijana hao kama vile Kigogo, Magomeni, Tabata, Manzese na maeneo ya Mbagala,wamepangwa askari wa kutosha wa doria ili kudhibiti mlipuko wowote wa vitendo vya kihuni vyenye ishara ya uhalifu vinanyoleta hofu kwa wananchi.
Kwa ujumla ni kwamba vijana hao hawana uwezo tena wa kufanya uhalifu katika makundi yao kutokana na mpango kazi uliopangwa na jeshi la Polisi Kanda maalum na kwa sasa tayari wamashakamatwa viongozi [Ring Leaders] [06] wa vikundi hivyo na majina yao ni kama ifuatavyo;
- ATHUMAN SAID Miaka 20 Mkazi wa Kigogo.
- JOSEPH PONELA Dereva Bodaboda,Mkazi wa Kigogo Mkwajuni.
- CLEMENT PETER Miaka 25,Fundi Seremala,Mkazi wa Kigogo.
- ROMAN VITUS Miaka 18,Mfanya biashara Mkazi wa Kigogo.
- MWINSHEHE ADAM Miaka 37, Mkazi wa Temeke Mashine ya Maji.
- DANIEL PETER Miaka 25,Mkazi wa Yombo.
Jeshi la polisi limewatoa hofu wananchi wa Dar es Salaam kwamba si kweli kuna tishio la vijana hao kama inavyosemekana kwani jeshi la Polisi limejiimarisha kiulinzi na vijana hao hawana uwezo wa kufanya watakavyo kama uvumi ulivyoenezwa kimakosa.
Uchunguzi umebaini kwamba chanzo cha uvumi huo ni kwamba tarehe 18/05/2014 na 20/05/2014 palitokea mauaji ya vibaka wawili waliohusishwa na makundi haya na kwamba kulikuwa na hofu kuwa baada ya mazishi ya vijana hao vijana wenzao wangeweza kulipiza kisasi ndio maana pakawa na uvumi wa jumbe mbalimbali zilizoleta hofu.
Mwisho kabisa jeshi la polisi limeomba wananchi wawe watulivu na waendelee na shughuli zao kama kawaida na waachane na uvumi huo.
0 comments:
Chapisha Maoni