Kocha David Moyes na kocha mchezaji wa klabu ya Manchester United Ryan Giggs wameripotiwa kutoelewana.
Imeripotiwa kwamba gwiji huyo wa United aligoma kuhudhuria mkutano wa benchi la ufundi na alimwambia kocha mwenzie msaidizi Phil Neville hakukuwa na haja ya kwenda kwenye mkutano huo kwa sababu kocha mkuu wa timu David Moyes hasikilizi ushauri wake.
Kwa mujibu wa jarida lenye ukaribu na
klabu ya Manchester United, Fanzine, Moyes ameripotiwa kutokuwa na mahusiano mazuri ya kiungo Micheal Carrick kutokana na mbinu anazomuelekeza akimlazimisha mchezaji huyo kuangalia video za kiungo wa Everton Leon Osman ili aige namna anavyocheza.
Hilo ni jambo ambalo Carrick amewaambia jamaa zake wa karibu kwamba linamkera, nae Rio Ferdinand inasemekana ametofautiana na Moyes juu ya kuiga mbinu za beki wa Everton Phil Jagielka.
Taarifa nyingine kutoka Fanzine ni kwamba baadhi ya wakurugenzi wa bodi ya klabu wamepeleka kwa wamiliki wa club hiyo wazo la kumbadili kocha huyo japokua Moyes bado anapewa sapoti na Sir Alex Ferguson pamoja na Bobby Charlton.
0 comments:
Chapisha Maoni