Text Widget

Recent Posts

Januari 16, 2014

ELIGIVER MUNISI“MWALIMU MWENYE NDOTO KUBWA ZA KUWA STAR KATIKA FANI YA MOVIES NA UANDISHI WA VITABU NCHINI”


                  Mjasiriamali na mtunzi wa vitabu mwenye ndoto kubwa katika kuingia katika tasinia ya filamu nchini Tanzania aishie maeneo ya Tabata Dar es salaam na kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia hiyo.
Alieleza hayo alipokuwa akihojiwa na “HISIA TZ”, kuwa alishawahi kufanya mazoezi ya uigizaji katika
kikundi cha uigizaji kaole,ambachoni zao la mastaa wengi wakubwa nchini akiwepo Ray na marehemu Steven kanumba mwaka 2008


                                                   mwalimu eligiver akiwa nje ofisini kwake
                   Alifanya hapo mazoezi mbalimbali ya uigizaji na alishindwa kuendelea na hii fani kutokana na shughuli za kimasomo katika shule ya sekondari Tegeta akiwa kidato cha sita na sasa amerudi rasmi na kuahidi watu wategemee mambo mazuri kutoka kwake.
Pia aliongeza kuwa“kwa sasa nipo katika maandalizi ya mwisho ya kitabu changu cha historia ya maisha yangu ambacho naamini kitawasisimua watanzania wengi kutokana na stori yenye kusimulia maisha halisi ya mtanzania”.,alisema.
Picha akiwa ofisini kwake
                    Vilelvile aliahidi kuwa kitabu hicho(ambacho hakuweza kukitaja jina) kitapatikana na stori nzima hapahapa,HISIATZ.BLOGSPOT.COM.

0 comments:

Chapisha Maoni