Desemba 07, 2013
MJANJA KANASWA,HATIMAYE AUNT LULU ATUNGWA MIMBA,"SOMA HAPA ZAID"
Posted on Jumamosi, Desemba 07, 2013 by Unknown
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
MSANII wa filamu, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’ baada ya kurukaruka sana, sasa inadaiwa ni mjamzito wa takribani miezi mitano.
Akilinyetishia Ijumaa juu ya ishu hiyo, rafiki wa karibu wa Anti Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, msanii huyo sasa amekuwa mtumiaji mzuri wa maembe mabichi huku magauni mapana yakiwa ndiyo mavazi yake.
“Mwanzo alikuwa anaficha lakini sasa siyo siri na mwenyewe ameona ni bora kuwataarifu ndugu na marafiki zake,” alisema mtoa habari huyo.
Katika kujua undani wa hilo, waandishi wetu walimsaka Anti Lulu na kufanikiwa kumuona akiwa na kitumbo chake lakini akaomba asipigwe picha ila akasema: “Mmechelewa kujua, mbona inakwenda mwezi wa tano sasa, mwenye mzigo mtamjua nikishajifungua jamani,”alisema msanii huyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni