Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’ cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya waigizaji wenzie wa Bongo Movie kugoma
kuhudhuria msiba wa baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine.
“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja, Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank na ntazidi kumshukuru,” alisema.
“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.”
Katika kipindi hicho pia, Wema alisema yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.
Balozi Issac Abraham Sepetu (71), alizikwa kikristo katika kijiji cha Mbuzini,mkoa wa Kusini Unguja October 30 ambapo mazishi yake yalihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohammed Shein pamoja na viongozi wengine.
Novemba 14, 2013
WEMA AWAJIBU BONGO MOVIE WALIOSUSIA MSIBA WA BABA YAKE
Posted on Alhamisi, Novemba 14, 2013 by Unknown
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni