Msanii bora wa Hip Hop kwa mwaka 2013, Kala Jeremiah ameweka hadharani kisa cha kusikitisha sana kuhusiana na maisha ya utoto wake na kusema kuwa, wakati alipokuwa mtoto mchanga kabisa, aliibiwa na watu wasiofahamika ambao walichukua jukumu la kumlea kwa miaka kadhaa kabla ya kukutana tena na mzazi wake pamoja na ndugu zake wengine.
Kala ambaye hakutaka kuzungumzia kisa hiki kwa undani zaidi amesema kuwa alipofikia umri wa miaka 16 ndipo alipokutana na mama yake mzazi, na kila anapokumbuka kisa hiki kinamfanya afikirie mambo mengi sana ambayo yanamuumiza.
Hata hivyo, msanii huyu ameahidi kuwa siku nyingine atakapokuwa sawa atajitahidi kuelezea wapenzi wa kazi zake kuhusiana na mchongo huu mzima wa kusikitisha na kusisimua kuhusiana na maisha yake ya zaman
Novemba 22, 2013
KALA JELEMIAH ATOBOA SIRI"FUATILIA"
Posted on Ijumaa, Novemba 22, 2013 by Unknown
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni