Text Widget

Recent Posts

Agosti 14, 2014

ALIYEKUWA KOCHA WA SIMA LOGA AONDOKA BONGO;TAZAMA PICHA AKIWA AIRPORT.


Wakati Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri raia wa Zambia ametua nchini, angalia aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zdravko Logarusic alivyoliaga jiji la Dar.Kupitia mtandao wa Facebook, Loga ametupia picha mbili huku akiandika “by by Tanzania), akimaanisha bye bye Tanzania.

Loga ameiaga Tanzania kwa picha hizo, moja akiwa ndani Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa amepiga shati lake la pink na mkononi ameshikilia kinywaji aina ya Redbull.
Picha ya pili, Loga anaonekana kiwa amekaa kwenye beki, hapo ni kabla ya kuingia ndani ya uwanja huo.
Kocha huyo ameondoka na dege la Shirika la Ndege la Tukish.
Kama safari yake imekwenda vizuri, tayari Loga atakuwa amewasili kwao salama.
 

0 comments:

Chapisha Maoni