ROSE MUHANDO AFIKISHWA POLISI
Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando
MWANAMUZIKI wa
nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo
cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar baada ya mchungaji mmoja wa
Kinigeria anayefanya shughuli zake nchini DR Congo, Kabagambe Tchanda
kumshitaki akidai kumlipa fedha ili akafanye onesho badala yake akaingia
mitini.
Uchunguzi
uliofanywa na paparazi ndani ya jeshi hilo, umegundua kuwa kuna madai
hayo na kwamba mchungaji huyo alitua jijini Dar na kufanya mazungumzo na
Rose kwa ajili ya kwenda kutumbuiza nchini DR Congo, Julai mwaka huu
katika mkutano uliohusisha wageni kutoka Ulaya na kukubaliana amlipe
Dola za Marekani 5,000 (zaidi ya shilingi milioni 8).
Kwa
mujibu wa chanzo, ilidaiwa kuwa mchungaji huyo alimkabidhi Rose dola
1,900 kama utangulizi na kubaki dola 3,100 ambazo angemlipa baada ya
onesho. Makabidhiano hayo yalifanyika Magomeni ya Mwembechai jijini Dar.
Kutokana
na sekeseke hilo, paparazi alimsaka mchungaji huyo na alipoulizwa kuhusu
kuwepo kwa madai hayo, alikiri na kusema alimuamini sana Rose lakini
cha ajabu mambo yamekuwa tofauti kwa kuwa hakufika kwenye tamasha.
Mchungaji
huyo aliendelea kudai kuwa, kinachomuuma zaidi ni kwamba, Rose hataki
kumrudishia fedha zake na badala yake amekuwa akimzungusha na chenga
kibao.
“Siamini
kabisa kama Rose angeweza kufanya vile maana yeye ni mtumishi wa Mungu,
sasa kwa nini afanye mambo yasiyompendeza Bwana? Nashangaa sana, sijui
hata ni nini kimemuharibu huyu! Nikimpigia simu akipokea kesho haziishi.
“Anashindwa
kuwa na utu maana mimi nimeishiwa fedha naishi kwa shida hapa nchini,
angenipatia hizo pesa zingenisaidia sana maana ujio wangu huu ni kwa
sababu ya kudai hizo pesa tu, ndiyo maana nikaamua kulifikisha suala
hili kwenye vyombo vya dola baada ya kuona hatuelewani,” alisema.
Ili
kuweka sawa mzani wa habari, paparazi alimtafuta Rose Muhando kupitia
simu yake ya mkononi ambayo iliita bila ya kupokelewa licha ya kumtumia
ujumbe mfupi wa maandishi aliamua kukaa kimya.
Kesi
imefunguliwa katika Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa
jalada namba KJN/RB/7122/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.
CHANZO:MATUKIO NA VIJANA
0 comments:
Chapisha Maoni