NA SYLVESTER
DAVID
MSANII
maarufu wa Hip Hop nchini, Golden
Mbunda, ‘Godzilla’ amewataka mashabiki wake kuwa tayari kwa ujio wa wimbo
mpya aliomshirikisha Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum’.
Aliyasema
hayo jana katika mazungumzo na Tanzania Daima kuwa mashabiki wake wawe tayari
kuupokea wimbo huo kwani umebeba ladha tofauti.
“Nina wimbo
wangu mpya na Diamond ambao wote tumechana utatoka muda si mrefu kutoka Mj
Records chini ya Marco Chali mashabiki wangu kaeni mkao wa kula”.Alisema
Msanii huyo aliyechini
ya usimamamizi studio za Mj Record zilizopo jijini Dar es salaam anayetamba na wimbo wa “Nisome” aliyewahi
kutamba na nyimbo mbalimbali zikiwemo Salasala, Kingzilla, The same, Get up my
way na lakuchumpa aliomshirikisha mchekeshaji maarufu nchini,Joti.
Alisema, kuna kanda
mseto nyingine ambayo inasimamiwa na na mwandaaji wa muziki nchini ‘Zaa
Chaa’ ambaye ni mdogo wa Marco Chali kutoka Studio za Mj Record iitwayo Watoto
wa Mama.
Pia
aliongeza kuwa wiki ujayo anaanza kufanya video ya wimbo wa‘ Nisome’ unaotamba katika vituo mbalimbali vya Redio nchini ambayo
itatoka muda si mrefu.
Mwisho…………
0 comments:
Chapisha Maoni